Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake






Ijue Idara ya Vijana

Jina la Idara ni Zanzibar International Christian Center - Christ's Ambassadors (CA's); Yaani ikiwa na maana ya Vijana mabalozi wa Kristo.'Kimsingi ni Idara ya Vijana'.

cas logo

MAONO

Maono ya Idara ya Vijana ni kua na Vijana:-

  • 1: Walio jaa Roho mtakatifu kikamilifu.
  • 2: Walio hamasika kihuduma.
  • 3: Wenye mzigo na uwezo wa kuvuna roho zilizopotea kwa ufanisi mkubwa.
  • 4: Kua na viongozi waaminifu na wawajibikaji katika ngazi zote.

DHIMA

idara ya Vijana wajumbe wa Kristo kwaajili ya: -

  1. Kuhamasisha vijana.
  2. Kuunganisha Vijana.
  3. Kulea vijana katika malezi bora.
  4. Kupandikiza vijana Mzigo na Maono ya; -
    • 1: Kuabudu kwa hiari yao baada ya kufundishwa umuhimu wa kumuabudu MUNGU.
    • 2: Kutumika kwa bidii na viwango vya juu.

MAKUSUDI

Makusudi ya Idara ni:-

  1. Kushuhudia.
    • Idara inawaandaa vijana kwa mafunzo mbalimbali na kuwahamasisha ili kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali waweze kufanya uinjilisti wenye Nguvu utawawezesha kuwaleta watu wenyedhambi kwa Yesu.

VIONGOZI WA IDARA YA VIJANA KANISA